Monday, June 18, 2012

AFRICA NEWS: UPANDE WA SHAFIQ NAO WATANGAZA KUSHINDA UCHAGUZI MISRI


Kambi ya Ahmed Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho katika utawala wa dikteta Hosni Mubarak nchini Misri imetangaza kuwa Shafiq anaongoza kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliofanyika Jumamosi na Jumapili.

Timu ya kampeni ya Shafiq imesema mgombea wake anaongoza kwa wingi wa kura na hivyo kupinga tangazo la hapo awali la harakati ya Ikhwanul Muslimin kwamba mgombea wake Muhammad Morsi ndiye aliyeshinda kwa kupata asilimia 52 ya kura. Hata hivyo, duru nyingi za habari zinaripoti kuwa Morsi ndiye anayeongoza. Matokeo rasmi yatatangazwa siku ya Alhamisi. Huku hayo yakijiri, Baraza la Kijeshi nchini Misri limetoa taarifa na kusema kuwa rais mpya atakuwa na madaraka ya wastani ikilinganishwa na Hosni Mubarak. Jeshi limesema Rais hatokuwa Amiri Jeshi Mkuu, rais pia hatoweza kuanisha bajeti ya nchi na kwamba mamlaka ya bunge lililovunjwa na mahakama yataendelea kubakia mikononi mwa jeshi.

No comments:

Post a Comment