Monday, June 18, 2012

MBEYA UPDATE: MTOTO AFARIKI MGODINI CHUNYA


M
wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimanjiwa na mkazi wa Kijiji cha Mlimanjiwa,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mussa Manyesa(9),amefariki dunia kwa kutumbukia katika shimo la maji katika mgodi unaomilikiwa na Mrs Kasaka wa wilaya hiyo na kusimamiwa na Isaack Msowoya.

Tukio hilo limetokea Juni 16 majira ya saa 10 jioni,wakati mtoto huyo akiwa na wenzake na alipopita kando kando ya shimo hilo alitumbukia na kupoteza maisha papo hapo.

Baba wa mzazi wa marehemu Bwana Leonard Manyesa,amesema wakati wa tukio hilo alikuwa nyumbani kwake na muda mfupi alipata taarifa za mwanae kufariki,hali iliyompelekea kufika eneo la tukio,kisha kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa kijiji Bwana Shaban Masa.

Polisi walifika eneo la tukio na kuthibitisha kifo hicho na kuwaruhusu ndugu wa marehemu kuuchukua mwili wa marehemu na mazishi ya kuuaga mwili huo yalifanyika Juni 17 mwaka huu  kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment