Tuesday, June 26, 2012

AFRICA NEWS: AL BASHIR AWATIMUA WASHAURI WAKE


Rais Omar al Bashir wa Sudan amewafukuza kazi washauri wake wote.
Rais wa Sudan amesema amechukua hatua ya kuwafukuza kazi washauri wake wote 9 katika utekelezaji wa mpango wa kubana matumizi ya serikali na uongozi bora wa nchi.
 
Ameongeza kuwa kipindi cha sasa nchini Sudan kinawalazimu Wasudani wote kufanya jitihada kubwa za kulinda maslahi ya nchi na kushirikiana na serikali. Hatua hiyo ya Rais wa Sudan imechukuliwa baada ya maandamano ya wiki iliyopita ya wananchi waliokuwa wakipinga suala la kupunguzwa bajeti ya serikali na kuzidishwa bei ya nishati, suala ambalo limewatia wasiwasi mkubwa wananchi. Baada ya Sudan Kusini kujitenga na Sudan, Khartoum ilipoteza asilimia 75 ya mapato ya mafuta na inakabiliwa na nakisi kubwa ya bajeti ambayo inapaswa kufidiwa kwa kubana matumizi

No comments:

Post a Comment