Thursday, June 14, 2012

URUSI KUKATWA ALAMA SITA KAMA WAKIENDELEA NA VURUGU.


 

KAMPENI Urusi za kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya michuano ya Ulaya 2016 zinaweza kukwama kabla hazijaanza baada ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya-UEFA kuitishia nchi kuinyang’anya alama sita katika michezo yake ya kufuzu michuano hiyo kama mashabiki wake wataendelea kufanya vurugu. UEFA pia wametoza nchi hiyo faini ya kiasi cha euro 120,000 baada ya mashabiki wa timu hiyo kufanya vurugu baada ya ushindi wa mabao 4-1 waliopata dhidi ya Jamhuri ya Czech Ijumaa iliyopita. Rais wa UEFA, Michel Platini amesema kuwa mashabiki wahuni ambao wanataka kuvuruga michuano hiyo kwa makusudi hawawezi kuvumiliwa na shirikisho hilo hivyo pia hatua zitachukuliwa dhidi yao kama wakibainika kushiriki moja kwa moja katika vurugu hizo. UEFA pia inaendelea kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea kabla na baada ya mchezo baina ya Poland na Urusi ambao walitoka sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment