Thursday, June 14, 2012

DI MATTEO APEWA MIKOBA RASMI YA KUINOA CHELSEA.


 

Hatimaye klabu ya Chelsea imemteua rasmi kocha Roberto Di Matteo kuinoa klabu hiyo katika kipindi cha miaka miwili ijayo baada ya kuipa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya pamoja na Kombe la Chama cha Soka nchini Uingereza-FA. Di Matteo ambaye alikuwa kocha wa muda wa klabu hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Andre Villas-Boas kutimuliwa kibarua hicho mwezi Machi mwaka huu na kufanikiwa kuingoza klabu hiyo ambayo ilikuwa ikisuasua kupata mafanikio hayo. Mara baada ya kuachiwa kukaimu nafasi ya Villas-Boas kocha huyo alipoteza michezo mitatu tu kati ya 21 ambayo timu hiyo ilicheza na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu hiyo waliunga mkono ateuliwe kama kocha wa kudumu wa klabu hiyo. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Di Matteo mwenye umri wa miaka 42 amesema kuwa amefurahishwa na suala hilo na kuongelea mafanikio ya kihistoria aliyopata katika klabu hiyo msimu uliopita na kuahidi kuyaendeleza katika msimu unaokuja wa ligi ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment