Tuesday, June 12, 2012

UINGEREZA HAWATAKUWA MABINGWA EURO 2012 - DESAILLY.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Marcel Desailly amesema kuwa timu ya taifa ya Uingereza haiwezi kushinda taji la michuano ya Kombe la Ulaya kutokana na mchezo wa sare ya bao 1-1 iliyotoka dhidi ya Ufaransa. Desailly mwenye wa umri wa miaka 43 ambaye amewahi kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka 1998 na taji la michuano ya Ulaya mwaka 2000 akiwa na kikosi cha Ufaransa alinukuliwa akisema kuwa kikosi cha Uingereza hakina nguvu za kunyakuwa taji la michuano hiyo. Nyota huyowa zamani mzaliwa wa Ghana ambaye pia amewahi kushinda taji la klabu bingwa ya Ulaya akiwa na vilabu vya Marseille na AC Milan amesema katika mchezo uliochezwa jana wameonyesha kabisa hawawezi kufika mbali kutokana na aina ya mchezo wa kujihami waliokuwa wakicheza. Katika ambaye katika mahojiano hayo pia Desailly alidai kuwa klabu ya Swansea inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza ilikuwa ikimhitaji lakini alikataa kwakuwa anahitaji changamoto kubwa zaidi amesema kuwa Ufaransa inakabiliwa na changamoto kubwa zaidi katika michezo inayofuata. Desailly alifafanua kuwa mchezo Ufaransa waliocheza dhidi ya Uingereza hauwezi ukawa kipimo kwa kikosi hicho kwakuwa haukuwa mchezo uliokuwa na upinzani mkubwa kiufundi ila kuna makosa madogo tu ya kurekebisha ili kukabiliana na mchezo unaofuata dhidi ya Ukraine ambao wameshinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Sweden kwa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment