Friday, June 1, 2012

UEFA YAMFUNGIA TERRY MECHI TATU.


 

BEKI wa Chelsea John Terry anatarajiwa kukosa michezo miwili ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao baada ya Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kumfungia michezo mitatu. Terry tayari amekosa mchezo mmoja wa fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich kufuatia kai nyekundu aliyopewa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Barcelona lakini UEFA imeamua kumuongeza mechi zingine mbili kutokana na adhabu hiyo. Mchezaji huyo sasa atakosa mchezo wa Super Cup wakati Chelsea ambao ni washindi wa kombe la klabu bingwa Ulaya watakapochuana na mabingwa wa ligi ya Ulaya au Europa League Atletico Madrid Agosti mwaka huu pamoja na mchezo wa kwanza wa timu hiyo katika msimu ujao wa ligi hiyo. Chelsea walishinda michuano hiyo pamoja na kuwakosa wachezaji wake nyota ambao walifungiwa wakiwemo Ramires, Branislav Ivanovic na Raul Meireles.

No comments:

Post a Comment