Wednesday, June 13, 2012

TANZANIA POLITICAL NEWS: BUNGE LA BAJETI LAANZA, LEO ZAMU YA WIZARA YA FEDHA


DODOMA
BUNGE la Bajeti limeanza juzi mjini Dodoma huku moja ya kazi ya bunge hilo ni kuwasilisha bajeti inayowafanya watanzania kuisubiri kwa hamu kubwa masikioni mwao.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa anatarajiwa kuwasilisha bajeti katika bunge hilo hii leo.

Agosti 22, mwaka huu bunge hilo linatarajiwa kumaliza vikao vyake.

Juni 22, Bunge litajadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2012ikiwemo na kuidhinisha sheria ya matumizi ya serikali wa mwaka 2012.

Juni 25 hadi 29, itasomwa hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa shughuli za serikali katika mwaka wa fedha unaomalizika na matarajio ya serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata.

Pia vipindi vya maswali na majibu kutarajiwa ikiwemo na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda

No comments:

Post a Comment