Wednesday, June 13, 2012

TANZANIA GOSPEL NEWS: VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA


''Inuka maana shughuli hii yakuhusu wewe, uwe na moyo mkuu, ukaitende(Ezra 10;4)''.
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA.

Siku 18 zimebakia kabla ya pazia la upigaji kura kufungwa kwa waimbaji wa gospel barani Afrika, ambao wanawania tuzo mbalimbali kupitia Africa gospel music awards ambazo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza. Ambapo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana mwimbaji wetu mmoja tu, ametutoa kimasomaso kwa kupendekezwa katika kuwania kupata tuzo hizo mwimbaji huyo si mwingine bali ni Christina Shusho, ambaye mwaka jana alitoka mikono mitupu lakini mwaka huu tukiungana kwa pamoja watanzania wote kwa kumpigia kura lazima atarudi na tuzo zote mbili alizopendekezwa kuwania.

Shusho yumo kwenye kuwania mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa mwaka Afrika ya mashariki, tuzo ambazo anawania na waimbaji wengine wanaofanya vyema kwenye gospel barani Afrika wakiwemo wakina Ntokozo Mbambo wa Afrika ya kusini na waimbaji wengine. Kikubwa ninachoweza kukwambia tukifanikiwa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kumpigia kura atakuwa nanafasi kubwa ya kutwaa tuzo hizo, kwasababu waimbaji wengine wanaowania tuzo hizo wengi wao wanatoka nchi moja hali ambayo itafanya kura zao kugawana kitu ambacho kitatupa nguvu ya kumwezesha Shusho kurudi na tuzo kwani Tanzania nzima kura zetu tunaelekeza kwake.


Mikakati mbalimbali inafanywa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika upigaji kura kwakuwa hauhitaji kulipa ili kupiga kura, kikubwa unatakiwa ujiandikishe kwenye tovuti ya shindano hilo ambayo maelekezo yake yapo chini ya habari hii, zaidi kama nilivyoandika mikakati inafanywa ili kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili katika siku 18 zilizobaki. Hapo jana bloggers walikutana na Christina Shusho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ili kupanga mikakati zaidi ya kuweza kupata tuzo hizo ambazo faida yake ni kumwinua Yesu pamoja na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania duniani. Natumai umenielewa ili kupiga kura ingia kwenye link hii na kufuata maelekezo chini yake.

No comments:

Post a Comment