Wednesday, June 6, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: UCHAGUZI YANGA NYOTA WA ZAMANI WAJITOKEZA KUGOMBEA


WACHEZAJI waliopata kuichezea klabu ya Yanga miaka iliyopita ni mingoni mwa wanachama waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu ya soka ya Yanga uliopangwa kufanyika Julai 15 jijini Dar es Salaam.
Leo ndio ilikuwa siku ya mwisho kurejesha foimu hizo ambapo wachezaji hao wa zamani waliojitosa ni pamoja na Aron Nyanda,  Ramadhan Mzimba, Edger Fongo, Zubeiry Katwila (ujumbe) na Ali Mayay anayewania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

No comments:

Post a Comment