Wednesday, June 6, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: OKWI KUUZWA AKISHINDA MAJARIBIO


SIMBA
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba inatarajiwa kumuuza nyota wake wa kimataifa Mganda Emmanuel Okwi kwa Euro 500,000, iwapo atafuzu majaribio yake katika klabu moja nchini Australia. 
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kwenda huko mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Kagame.

Alisema dau hilo pia litahusisha timu yoyote itakayomuhitaji mchezaji huyo ambapo mbali na Australia tayari kuna timu kutoka Serbia, Uingereza na Afrika Kusini zimeonyesha nia ya kumsajili nyota huyo.
‘habari nzuri ni kwamba uongozi umekuwa ukipokea maombi toka nchi tofauti zikiwemo hizo...sisi hatuna hiyana bwana ili mradi tu wawe na kiasi cha fedha kisichopungua Euro 500,000,’alisema.

No comments:

Post a Comment