T |
aifa Stars imewasili Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.

Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment