Wednesday, June 20, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: AZAM YAANZA MAZOEZI KUJIFUA LIGI KUU NA KOMBE LA SHIRIKISHO


K
LABU ya Azam FC inaendelea vema na maandalizi yake ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame na leo asubuhi walifanya mazoezi katika ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam.

Azam ilianza mazoezi ya viungo na kusaka pumzi na stamina wiki mbili zilizopita, Beach na Gym na wiki wanatarajiwa kuanza kuuchezea mpira.

Tayari Azam, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wamekwishamalisha usajili wa wachezaji wao hata kabla ya kwenda likizo.Programu ya maandalizi ya Kombe la Kagame, inayoendelea hivi sasa itamalizika siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo, Juni 28 na yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.Maandalizi kwa ajili ya VPL yatahusisha pia ziara ya nje ya nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema nchi hiyo itatajwa baadaye.

Wachezaji wapya kikosini Azam msimu huu ni kiungo Mkenya George ‘Blackberry’ Odhiambo na kipa Deogratius Munishi kutoka Mtibwa Sugar, wakati Aishi Salum, Jackson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga, wamepandishwa kutoka akademi ya Azam.

Kikosi kamili cha Azam FC kinaundwa; na makipa, Mwadini Ally, Deo Munishi ‘Dida’ Aishi Salum na Jackson Wandwi, mabeki wa Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samir Haji Nuhu, Luckson Kakolaki, Said Mourad, Joseph Owino na Aggrey Morris.

Viungo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadalla, Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche, Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati washambuliaji ni Gaudence Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’.

Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza Kombe la Kagame, baada ya kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu. Katika Kombe la Kagame mwaka huu, wenyeji Bara wataingiza timu tatu, Yanga ambao ni mabingwa watetezi, wakati Simba na Azam wanaingia kwa nafasi za uwakilishi.

Imeandikwa na Prince Akbar, Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment