Wednesday, June 20, 2012

TANZANIA BOXING NEWS: PAMBANO LA CHEKA NA MMALAWI LAOTA NYASI


P
ambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na  Mmalawi John Massamba lililokuwa lifanyike Ijumaa, limeahirishwa mpaka hapo tarehe itakapotajwa tena kuwa miyayusho atacheza na nani, lini na wapi. 

Haya yamekuja kutokana na  bondia John masamba toka Malawi akiwa hana hadhi
ya kucheza na miyeyusho na wasiwasi wa afya yake,bondia huyo toka
Malawi mwenye rekodi ya mapambano ya kupigwa mawili na kushinda
mawili,amecheza mwaka 1969, inaonekana ni mbovu na rekodi yake ya
utata ukilinganisha na miyeyusho mwenye mapambano 42 ya kueleweka.

Kutokana na utata huo wa bondia wa malawi na kutokamilisha malipo na
vibali vyote toka Utamaduni na michezo,
Hivyo mpambano umesitishwa mpaka taratibu zitakapokamilika za upande
wa vibali na  kumleta bondia mzuri wa kucheza na Francis
miyeyusho.mapambno mengine yatakuwepo kama kawaida katika ukumbi wa
Dar live kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba.

No comments:

Post a Comment