Saturday, June 2, 2012

SUPER CUP SASA KUCHEZWA CHINA.

SHIRIKISHO la soka nchini Hispania-RFEF limefikia makubaliano ya awali na kampuni moja nchini China kusimamia mchezo wa ufunguzi kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Hispania au Super Cup ambao utafanyika jijini Beijing kuanzia 2013. Taarifa kutoka shirikisho hilo imesema kuwa mchezo huo ambao huwakutanisha bingwa wa Ligi Kuu ya nchini humo pamoja na mshindi wa Kombe la Mfalme utakuwa ukichezwa katika Uwanja wa Bird Nest uliopo katika mji mkuu wan chi hiyo, Beijing. Ingawa katika taarifa hiyo iliyotumwa katika mtandao wa RFEF haikufafanua kiasi ambacho watapa kwa ajili ya mpango huo lakini vyombo vya habari nchini Hispania vimesema kuwa mpango huo ambao utakuwa wa miaka mitano utaipatia RFEF kiasi cha euro milioni 40. Timu ya taifa ya Hispania inatarajiwa kucheza na China katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kutetea ubingwa wao wa Kombe la Ulaya Juni 10 ambapo watacheza na Italia jijini Gdansk, Poland.

No comments:

Post a Comment