Monday, June 11, 2012

POLISI WAMUOKOA OBODO.

POLISI nchini Nigeria jana usiku walifanikiwa kumuokoa kiungo kimatifa wa Nigeria na klabu ya Udinese Christian Obodo ikiwa ni siku toka alipotekwa katika mji wenye utajiri mkubwa wa mafuta uliopo kusini mwa Delta. Msemaji wa Polisi wa jimbo la Delta Charles Muka amesema kuwa polisi wa hapo walifanikiwa kumuokoa Obodo na kuwakamata baadhi ya watu wanaotuhumiwa kufanikisha utekaji huo ambao walikuwa hawajafanikiwa kuondoka katika jimbo hilo kwa kuzifuatilia simu ambazo watekaji hao walikuwa wakitumia. Watekaji walifanya mawasiliano na familia ya mchezaji huyo inayoishi Warri ambaye alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Lecce ya huko Italia wakidai fidia ya dola 187,500. Utekaji umekuwa ni suala la kawaida katika jimbo hilo ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta ambapo magenge ya watekaji yamekuwa kwa kawaida wakiwateka wafanyakazi wa kigeni wanaofanya kazi katika eneo hilo. Lakini katika kipindi cha karibuni watekaji hao wamekuwa wakiteka familia na wachezaji wa mpira wa nchi hiyo ambapo katika kipindi cha karibuni baba wa kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo na klabu ya Chelsea John Mikel Obi alitekwa ambapo watekaji walidai kiasi cha dola bilioni nne.

No comments:

Post a Comment