Monday, June 11, 2012

POLAND IMEFANYA KAZI KUBWA KUZUIA UBAGUZI - GULLIT.

MCHEZAJI nyota wa zamani wa Uholanzi, Ruud Gullit amesisitiza kuwa nchi Poland imefanya juhudi kubwa kupambana na matukio ya kibaguzi kuelekea katika michuano ya Ulaya mwaka huu pamoja na mjadala kuhusiana na suala hilo unaendelea hivi sasa. Kuna taarifa kuwa baadhi ya wachezaji wa Uholanzi walipigiwa kelele za kibaguzi wakati wa mazoezi yao jijini Krakow wakati mchezaji wa Jamhuri ya Czech Theodor Gebre Selassie kuna tuhuma kwamba alifanyiwa kitendo cha kibaguzi wakati timu yake ilipokubali kipigo kutoka kwa Urusi jijini Wroclaw jana. Pamoja na matukio hayo Gullit amesema kuwa ameitembelea nchi mara nyingi na amekuwa akiona juhudi zilizokuwa zikifanywa kupambana na suala hilo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya. Nyota huyo wa zamani aliendelea kusema kuwa ameona juhudi ambazo zimefanywa na Poland hivyo moja kwa moja anarejea kwa mashabiki wanaoshuhudia michuano hiyo kuachana na vitendo hivyo ambavyo sio vya kibinadamu katika dunia ya sasa na kuzishangilia timu zao.

No comments:

Post a Comment