Tuesday, June 5, 2012

PELE AKIPONDA KIKOSI CHA MENEZES.


 

NYOTA wa zamani wa Brazil, Pele amekiponda kikosi cha timu ya taifa ya nchi kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki mwaka huu kwa kudai kuwa hakipo tayari kwa ajili ya michuano hiyo kufuatia kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mexico mchezo ambao ulifanyika jijini Texas, Marekani. Pele amesema kuwa ni jambo zuri timu hiyo kufungwa katika kipindi hiki ambacho watu walikuwa wanadhani kikosi hicho tayari kwa ajili ya michuano hiyo kufuatia kuifunga timu ya taifa ya marekani mabao 4-1 katika mchezo uliotangulia. Nyota huyo ambaye alikuwa mkali ya kuzifumania nyavu enzi zake aliendelea kusema kuwa kikosi hicho ni kizuri na kina wachezaji wazuri lakini bado hakiko tayari kupambana na hali ngumu kama waliyopata katika kipigo cha juzi hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Kocha wa timu hiyo Mano Menezes anaamini kuwa atakiongoza kikosi hicho kunyakuwa medali ya kwanza ya olimpiki katika michuano itakayofanyika Agosti mwaka huu jijini London, Uingereza.

No comments:

Post a Comment