Tuesday, June 5, 2012

MISSION ACCOMPLISH AT CHLESEA - DROGBA.


 

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea, Didier Drogba amesema kuwa kazi kubwa katika maisha yake ya soka ameimaliza baada ya timu yake kushinda michuano ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu ya Bayern Munich mwezi uliopita. Drogba mwenye umri wa miaka 34 aliwaambia waandishi wa habari nchini kwao kuwa taji hilo linamaliza mbio zao za muda mrefu za klabu hiyo kuliwania na anawapongeza wachezaji wenzake pamoja na makocha ambao wamewezesha hilo kufanikiwa. Mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast aliendelea kusema kuwa kushinda taji la ligi ya mabingwa ni kukamilisha kazi kubwa ambayo ilimpeleka katika klabu hiyo na kwa kupindi kirefu wamekuwa wakikaribia kufanya hivyo lakini anadhani wakati wao ulikuwa haujafika. Drogba pia alizungumzia penati ya mwisho aliyopiga dhidi ya Bayern Munich na kuiwezesha timu yake kunyakuwa taji hilo na kudai kuwa katika muda ule ilibidi aondoe mawazo yote yakiwemo ya kukosa penati katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika hali ambayo ilimuwezesha kupiga penati ile kwa kujiamini na bila woga ndio maana akashinda kirahisi. Drogba aliyewahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mara mbili ambaye muelekeo wake baada ya kuikacha Chelsea bado haujajulikana alitangaza kuwa atastaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment