Sunday, June 24, 2012

NASRI AZOZANA TENA NA WAANDISHI.


 

KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri ameingia katika mgogoro mwingine na waandishi wa habari wa nchi yake kufuatia kutolewa kwa nchi yake kwenye robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Hispania. Nasri ambaye alikuwa anapita eneo la karibu na chumba cha mahojiano cha waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo ambapo alipoulizwa na mwandishi mmoja kuwa anajisikiaje baada ya kung’olewa kwenye michuano hiyo mchezaji huyo alionekana kujibu swali hilo kwa jazba. Nasri ambaye aliingia katika kipindi cha pili akitokea benchi la wachezaji wa akiba amekuwa na mahusiano yasiyo mazuri na vyombo vya habari vya Ufaransa katika michuano hiyo inayofanyika Poland na Ukraine. Baada ya kushinda bao la kusawazisha dhidi ya Uingereza katika mchezo wa kwanza Nasri alikuwa akikimbia kushangilia huku akiwa ameweka kidole katikati ya midomo yake akimaanisha kuwa wafunge mdomo, suala ambalo alifafanua baadae kuwa ujumbe huo ulikuwa ukienda kwa mwandishi wa Ufaransa ambaye amekuwa akikosoa kuitwa kwake katika timu hiyo.

No comments:

Post a Comment