Watu watatu wenye asili ya Ethiopia wamekamatwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kuwa kuingia nchini bila kibali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema wahabeshi hao walikamatwa majira ya saa 1 jioni juzi maeneo ya Uyole Jijini Mbeya.
Taarifa hiyo imewataja waliokamatwa kuwa ni Murugeta Dejene (28), Masele Fuge (22) na Kakere Tadeos (25) na kuongeza kuwa wahabeshi wengi wanaokamatwa nchini ni wale wanaokimbia ukame na njaa pia vita.
Aidha taarifa hiyo imesema watuhumiwa wapo mahabusu wakisubiri taratibu za kukabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment