Thursday, June 21, 2012

EURO 2012 NEWS: URENO YATINGA NUSU FAINALI


Cristiano Ronaldo ameiwezesha Ureno kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya EURO 2012 usiku wa kuamkia leo.
Hivyo Ureno anamsubiri mshindi atakayepatikana kati ya Hispania na Ufaransa. Robo  fainali  ya  kwanza  katika  mashindano  ya  kandanda  ya kuwania  taji  la  ubingwa  wa  mataifa  ya  ulaya , Euro  2012 imekamilika  kwa   Ureno  kuingia  nusu  fainali. Goli  lililowekwa wavuni  na  Cristiano  Ronaldo  lilitosha  jana  kuwafungisha virago  Jamhuri  ya  Czech  na  kuyaaga  mashindano  haya. Ureno imekuwa  timu  ya  kwanza  kuingia  katika  nusu  fainali  ya mashindano  haya. Leo  jioni  kutakuwa  na  patashika  nyingine, wakati  Ujerumani itakapominyana  na  Ugiriki, ambayo  ina  nia  ya  kuonyesha kuwa  matatizo  ya  kiuchumi  yaliyoko  nchini  humo hayaingiliana  na  soka.  Kansela  wa  Ujerumani  Angela  Merkel ambaye  ni  shabiki  mkubwa  wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani anatarajiwa  kuhudhuria   pambano  hilo  jioni  ya  leo. Merkel hakuhudhuria  mapambano  ya  timu  hiyo  katika  awamu  ya makundi  yaliyofanyika  nchini  Ukraine.

No comments:

Post a Comment