Friday, June 15, 2012

MBEYA UPDATE: SERIKALI YATAKIWA KUONGEZA NGUVU KUSIMAMIA HAKI ZA WATOTO


Kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika ni Kesho kwa Mataifa yote barani Afrika yaliyo chini ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo leo Jijini Mbeya Shirika lisilo la kiserikali la Child Support Tanzania limefanya matembezi ya Hiari kuadhimisha siku hiyo.
Katika Matembezi hayo ya hiari yamewajuimuisha watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu, wanafunzi wa shule za msingi, wazazi na walezi na jamii kwa ujumla huku mgeni wa heshima akiwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini John Mwela.

Askofu Mwela ameitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza nguvu katika kuangalia na kuzitktltza haki za watoto na wale walio na ulemavu ili kuleta usawa katika jamii.

Askofu Mwela amesema Serikali imekuwa ikijitahidi  kuwahudumia wenye ulemavu na watoto kwa kiasi kidogo  kwa kuwapatia elimu licha ya juhudi hizo kutozaa matunda kwa kiwango kikubwa hali amabayo imeendelea kuwatesa watoto hasa wenye ulemavu.

SUALA LA NDOA ZA JINSIA MOJA
Mbali na hilo Askofu Mwela amezungumzi msimamo wa Kanisa la Anglikana katika masuala yahusuyo ndoa za jinsia moja kwa kusema msimamo wao ni kutoziruhusu kabisa kwani ni kinyume na makusudi ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.

Hata hivyo ameweka bayana kuwa ni suala la mtu mwenyewe kujiamulia mwenyewe na kwambaUingereza yenyewe imeamua kufanya kufuru hiyo lakini sio Tanzania na watu wake.
Juni 16, 1976  watoto zaidi ya 6,000 waliuawa nchini Afrika kusini katika mji wa Soweto walipokuwa wakidai haki zao ambapo hujulikana kama “ MAUAJI YA SOWETO”.

No comments:

Post a Comment