Friday, June 15, 2012

KLINSMANN ACHOMOA KUINOA TOTTENHAM.

KOCHA wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann anakuwa kocha wa kwanza kukataa kibarua cha kuinoa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza baada ya kusisitiza kuwa hana mpango wa kuikacha nchi hiyo kwasasa. Klinsmann ambaye alikuwahi kuwa mshambuliaji nyota wa Ujerumani ndio alikuwa akipewa nafasi ya kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha Tottenham Harry Redknapp ambaye alitimuliwa wiki iliyopita. Katika miaka ya 1990 Klinsmann amewahi kuwa mshambuliaji wa Tottenham akiwa ameichezea klabu hiyo michezo 56 na kupachika wavuni mabao 33 katika misimu miwili aliyokuwepo White Hart Lane. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Klinsmann amesema kuwa bado hajapata mawazo ya kuondoka Marekani mpaka atapohakikisha ameiwezesha kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment