Tuesday, June 26, 2012

MBEYA UPDATE: MWALIMU MSTAAFU AHAMIA CHADEMA


MWALIMU mstaafu  wa elimu ya msingi mkoani Mbeya Bw.Paul  Lyambwa Mbamba (74) mkazi wa kijiji cha Lusungu katika Halmashauri ya Wilaya ya  Mbeya,  hivi karibuni alikabidhiwa kadi ya uanachama wa Chadema baada ya kurudisha kadi ya CCM chama  alichokitumikia tangu mwaka 1977
Bw.Mbamba amesema ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kuchoshwa na  CCM kwa vitendo vya unyanyasaji  ambavyo amevivumilia kwa kipindi kirefu wakati akikitumikia Chama hicho. Katibu wa CHADEMA tawi la Lusungo Bw.Gabriel Songa  amethibitisha kuwa ,Bw.Mbamba  alirudisha kadi yenye Na.155861 ya CCM ambayo alikuwa ameilipia ada  kwa mara ya mwisho mwezi Machi 25 mwaka 2010 kwenye tawi la Kasale kijiji cha Idiga kilichopo kwenye kata ya Bonde la Songwe jimbo la Mbeya Vijijini. Bw.Songa amesema kuwa,Bw.Mbamba ambaye   ana taaluma ya ualimu baada ya kukabidhi kadi hiyo ya CCM alikabidhiwa kadi ya CHADEMA yenye Na.CDM 0443364 mnamo Mei 26 mwaka huu na kuthibitisha kwamba Bw.Mbamba tayari amekuwa mwanachama hai wa Chadema Bw.Mbamba amesema kuwa ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanajifanya miungu watu ambapo wanataka kunyenyekewa na kukiendesha chama katika misingi ya urafiki na undugu kitendo ambacho kinasababisha wananchi kuongozwa na watu ambao si chaguo lao.

Mwalimu huyo amesema kwamba ,kwenye uanachama wake ndani ya CCM aliwahi kugombea nafasi ya udiwani katika kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu uliopita ambapo alisema kuwa alifanyiwa kitu mbaya vikiwemo vitendo vya kutishia uhai wake ambavyo vilikuwa vikifanywa na wanachama wa CCM  hata kusababisha kutupwa katika uchaguzi huo.Ameongeza kuwa ndani ya CCM hakuna Demokrasia ya kweli bali imejaa unafiki na vitendo vya ubabe ambavyo havina tija katika shughuli za maendeleo ya watanzania.

No comments:

Post a Comment