Tuesday, June 26, 2012

MBEYA UPDATE: DIWANI WA KATA AAMURISHWA NA WANANCHI KUHAMA MAKAZI YAKE


D
IWANI wa kata ya Bonde la Songwe kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya  kupitia CCM  Bw. Amon Mwakapala na wenzake wanne  
wametakiwa kuyahama  makazi  yao mara moja kufuatia tuhuma za maua
ji yaliyotokea mwaka jana  katika kijiji cha Lusungu mkoani hapa.


Maamuzi  hayo  yametamkwa hivi karibuni na baraza la  wazee wa vijiji
vya  Isambya,Lusungu na Malowe walioitisha  mkutano wa hadhara ili
kutoa tamko hilo hadharani kwa maelezo kuwa hawana imani na Mheshimiwa
Diwani  huyo pamoja na wenzake.

Chifu  wa kijiji cha Isambya anayefahamika kwa jina la Bw.Kayobile
Mwaveya katika mkutano huo uliohudhuriwa na wananchi wa vijiji hivyo
,amesema kuwa imani imetoweka katika vijiji hivyo kufuatia mauaji  ya
mkazi mmoja wa kijiji cha Lusungu  aliyetajwa kwa jina la Bw.Mwambunga
yaliyotokea  mwezi Novemba mwaka jana.

Kufuatia tuhuma hizo,watuhumiwa walikamatwa  na Jeshi la Polisi na
kufikishwa katika kituo cha kati mjini hapa na baadae kufikishwa
mahakamani ambako walisomewa  shitaka la mauaji.

Tuhuma hizo zimeibuka upya baada ya watuhumiwa hao kuachiwa huru mwaka
huu kitendo ambacho wakazi wa vijiji hivyo hawakubaliani nacho kwa
maelezo kwamba ,upo ushahidi wa wazi ambao unaonyesha watuhumiwa hao
walihusika na mauaji hayo .

Wananchi hao wamesema kuwa katika kesi hiyo hakuna haki iliyotendeka
kwa madai kuwa kuna mkono wa mtu huku wakimtaja mheshimiwa Mbunge na
mwenyekiti wa Halmshauri hiyo kupenyeza mkono wao ili kuhakikisha
diwani huyo anaachiwa huru ,hivyo katika mazingira hayo uamuzi wao
umefikia kikomo cha kuwataka watuhumiwa hao waondoke kwenye makazi
yao.


Naye mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Mheshimiwa Luckison Mwanjale
ametajwa kumegewa ekari 14 kwenye eneo hilo la Umma ambalo walisema
tayari ameweka mawe ya kumiliki wakati wananchi hawana taarifa za
uzwaji wa eneo hilo .

Bw.Mwanjale ambaye yuko mjini Dodoma kwenye vikao vya Bunge,
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alikiri
kumiliki eneo la ekari 14 huko Malowe ambazo alizitolea maelezo kwamba
eneo hilo alilinunua kabla ya yeye kuwa Mbunge.

Aidha,amekiri pia kuwa  ni kweli  Diwani Mwakapala na hao wenzake
walikumbwa na tuhuma hizo huku akikataa katakata kumsaidia diwani huyo
 katika tuhuma hizo kama  ambavyo wananchi wa vijiji hivyo wamekuwa
wakimtupia lawama Bw.Mwanjale.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Bw.Andason
Mwakabenga alisema anazo taarifa zinazo husiana na mheshimiwa Diwani
Bw.Mwakapala,taarifa ambazo zilikuwa zikimtuhumu kujihusisha na mauaji
kisha kufikishwa mahakamani ambako aliachiwa huru naye pia alisema
hakuna msaada wake kwenye kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment