Monday, June 18, 2012

MBEYA UPDATE: KOCHA MAKA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUIPA NGUVU TIMU YA COPA COCA COLA

K
ocha wa Timu ya Copa Coca Mkoa  wa Mbeya amewataka wadau wa Soka Mkoani Mbeya kujitokeza kwa wingi kuisaidia timu yao kwa hali na mali.

Katika mahojiano wa JAIZMELALEO mchana wa leo Maka Mwalwisi amesema Kikosi cha safari hii ni kizuri chenye wachezaji wenye uwezo ukilinganisha na miaka mingine aliyowahi kuinoa timu hiyo.

Kocha Mwalwisi amesema utezi wa wachezaji 20 umezingatia kila kitu kinachohitajika katika michuano hiyo ya COPA COLA kwani kwa miaka mingine nichini Tanzani kumekuwa kukijitokeza vitendo vya ukiukwaji wa Sheria za Michuano hiyo.

Amesema kuwa ukiukwaji wa sheria za michuano hiyo umekuwa ukijitokeza katika umri wa wachezaji ambapo amesema katika timu yake hakuna kitu kama hicho.

No comments:

Post a Comment