Friday, June 22, 2012

MBEYA UPDATE: KICHANGA KINGINE CHAOKOTWA SOWETO

K
atika hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo akiongea na baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai kwamba kuna dispensary jirani hapo ambayo hawakutaka sema ni hospital ipi ambapo wana wasi wasi kwamba hutoa Mimba mabinti na kuwatupa eneo hilo.

Mbeya yetu tunafanya uchunguzi wa kina kama ni kweli maelezo ya wadau na tunafuatilia kama kweli Dispensary hiyo ipo

Imeandikwa na Joseph Mwaisango, Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment