Monday, June 18, 2012

MBEYA UPDATE: JAMII WA WAFUGAJI BONDE LA SONGWE KUONANA NA PINDA


W
AKATI vikao vya bunge la bajeti vikiendelea mkoani Dodoma, umoja wa wafugaji wa bonde la Songwe wilayani hapa,wameazimia kwenda mjini humo, kabla ya Julai 10 kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda, na kumueleza malalamiko yako dhidi ya viongozi wa Halmashauri hiyo na Jeshi la polisi yanayotokana na ukamataji wa mifugo.

Hatua imekuja baada ya wafugaji hao kuituhumu halmashauri hiyo na jeshi la polisi wilayani Chuna, kuigeuza jamii ya wafugaji kuwa kitega uchumi kwa kujipatia fedha kutokana na tabia ambayo imejengeka ya kuwakamata na kuwatoza faini za mamilioni ya fedha wafugaji kwa kile kinachodaiwa kuvunja sheria za mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika mji mdogo wa Mkwajuni, wilayani Chunya, Mwenyekiti wa Umoja huo, Julias Ngassa, amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa viongozi hao hawana nia njema na wafugani kwa kuwa vitendo vya ukamataji wa mifugo yao vimegeuka ni miradi ya wao kujiingizia fedha.

No comments:

Post a Comment