Thursday, June 21, 2012

MBEYA UPDATE: HALMASHAURI YA JIJI YATOA VIFAA KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO VYA SOKO

HALMASHAURI  Ya Jiji la Mbeya imetoa vifaa vya zaidi ya TZS 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Soko la Sokoine.
Hatua hiyo imefuatia mara baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kutaka kugoma kutoa ushuru wa biashara zao.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga ametoa vifaa hivyo mchana wa leo katika soko hilo ili ujenzi huo uanze mara moja kwani mpaka sasa Jiji limetoa zaidi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kugharimia ujenzi wa vyoo hivyo.

Mstahiki Meya Kapunga amesema kutokuwa na vyoo vya uhakika ni kuyatafuta magonjwa na vifo katika jamii ya wakazi wa Mbeya na kuwaasa pindi ujenzi huo utakapokamilika mapema mwishoni mwa mwezi ujao wafanyabiashara hao wanapswa kuvitunza kwa umakini ili vidumu zaidi.

No comments:

Post a Comment