Tuesday, June 12, 2012

MBEYA UPDATE: CHADEMA YAANZA MAFUNZO KWA MADIWANI WAKE


C
hama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kimeanza kuendesha mafunzo kwa madiwani wa Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwa na madhumuni ya kuwaongezea Uwajibikaji katika Kata zao.
 SINGO KAGAIRA BENSON
 LAZARO TITUS MASAI
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Waandishi Habari leo mchana katika Ukumbi wa Dk. Shein Jijini Mbeya Mkurugenzi wa Oganaizesheni ya Mafunzo CHADEMA Taifa  Singo Masala Makali Kigaira Benson amesema Mbeya ni miongoni mwa vituo 9 vilivyoteuliwa nchini kundesha mafunzo hayo.

Kigaira Benson amevitaja vituo vingine kuwa ni Kigoma, Mwanza, Kagera, Musaoma, Shinyanga, Moshi, Arusha na Kibaha ambapo kituo cha Mbeya kinawaleta pamoja madiwani wa chama hicho cha upinzani kutoka mikoa ya Ruvuma, Iringa, Rukwa na Mbeya.

Pia amesema CHADEMA hadi sasa ina madiwani 485 nchi nzima hivyo kwa kuwa wanajiandaa kuchukua dola ni vyema wakawafundisha viongozi wao kwa manufaa ya jamii baada ya kuchukua nchi mwaka 2015.

Kwa upande wake Lazaro Titus Masai, Mjumbe wa Kamati kuu Taifa ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu amesema wamejifunza kutoka nchini Ethiopia ambako Chama cha Upinzani kilifanikiwa kushika dola wakati fulani lakini kutokana kutojiandaa baada ya miezi 3 wakaikimbia ikulu.

Aidha Lazaro ameongeza kusema Ikulu yao ya Kwanza ni Kitongoji hivyo kuwapa mafunzo madiwani hao na viongozi wengine wa CHADEMA ni kuendeleza harakati waliyoianza ya Movement for Change (M4C).

No comments:

Post a Comment