Friday, June 8, 2012

MBEYA UPDATE: AFA KWA KUANGUKIWA NA MAGOGO


MTU mmoja amefariki dunia mkoani Mbeya baada ya kuangukiwa na magogo ya Mbao alipojaribu kuruka kutoka katika gari la mizigo lililokuwa likikaribia kupinduka.

Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Majaliwa Mbogella amesema tukio hilo limetokea Juni 7 mwaka huu majira ya saa 2:30 asubuhi katika kijiji cha Lualanje wilayani Chunya likihusisha gari yenye namba T 732 BWV aina ya Fuso.

Mbogela amemtaja marehemu katika tukio hilo kuwa ni Sani Mgavi(28) mkazi wa Mufindi mkoani Iringa aliyekuwa mkulima na pia fundi wa kupasua mbao .

Amesema Mgavi amekutwa na mauti baada ya kuangukiwa na magogo ya mbao yaliyokuwa yakisafirishwa na gari aliyokuwa amepanda lakini walipofika katika kijiji cha Lualanje gari hiyo ilikwama kwenye mchanga na kulalia upande.

Kufuatia hali hiyo,fundi huyo aliyehisi gari inapinduka aliamua kuruka na kwakuwa alirukia upande lilikolaria gari magogo yalimporomokea na kukatisha uhai wake papo hapo.

No comments:

Post a Comment