Friday, June 8, 2012

TANZANIA SOCIAL NEWS: WAISLAMU WAANDAMANA

Waislamu nchini Tanzania wameandamana mjini Dar-es-Salaam kwa lengo la  kuishinikiza kamati ya Baraza la Kitaifa la Mitihani NECTA kujiuzulu kufuatia tuhuma kuwa inawafelisha wanafunzi wa dini ya Kiislamu.
Waislamu waliandamana huku wakiwa na mabango yenye kutaka watendewe haki ambapo wamelaani vikali baraza hilo la mitihani na wamelitaka lijiuzulu. Mapema jeshi la lilikuwa limepiga marufuku maandamano hayo ya Waislamu. Siku chache zilizopita pia, Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa bin Shaaban Simba kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA alimtaka Katibu Mkuu wa NECTA, Dk Ndalichako ajiuzulu kufuatia kashfa hiyo ya kuhujumiwa matokeo ya mitihani ya wanafunzi Waislamu.

No comments:

Post a Comment