Wednesday, June 13, 2012

MAOFISA WA SOKA CHINA WAHUKUMIWA VIFUNGO JELA.

Xie Yalong.
WALIOKUWA maofisa wa zamani wa Ligi Kuu nchini China wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 na nusu kila mmoja baada ya kupatikana makosa ya kula rushwa na kufanya kuwa viongozi wa kwanza katika soka kuwekwa lupango ulemwenguni. Maofisa hao wa zamani ambao ni Nan Yong ambaye mbali na kifungo hicho pia ametozwa faini ya dola 31,400 na Xie Yalong ambaye yeye baadhi mali zake zitataifishwa kutokana na hukumu hiyo. Nan ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa 17 ya kupokea rushwa alihukumiwa katika mahakama ya Tieling iliyopo Kaskazini-Mashariki mwa China wakati Xie alikuhukumiwa katika mahakama Dandong pamoja na kukataa mashtaka yake aidai kuwa akiriki kufanya hivyo kwakuwa alikuwa akiteswa. Mbali na maofisa hao China ambayo imeamua kuongeza nguvu kupambana na masuala ya rushwa pamoja na upangaji wa matokeo ya mechi pia imewahukumu miaka sita jela wachezaji wanne wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo kwa makosa kama hayo.

No comments:

Post a Comment