Wednesday, June 13, 2012

LIGI KUU NCHINI KUCHEZWA BILA MASHABIKI VIWANJANI.

MWENYEKITI wa Baraza la Michezo nchini Misri, Emad Al Banani amebainisha kuwa msimu ujao wa 2012-2013 wa Ligi Kuu ya nchini humo huenda ikachezwa bila ya mashabiki kuhudhuria viwanjani. Katika mkutano na waandishi wa habari Banani amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa baadhi ya mapendekezo ambayo walitaka yafanyike kabla ya kuruhusu mashabiki kuingia viwanjani kama ilivyokuwa kawaida. Aliendelea kusema kuwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-EFA limefanya kazi kubwa kuhakikisha usalama katika viwanja na katika miezi michache ijayo wanatarajia kuweka mageti ya umeme pamoja na kamera yote hayo kwa ajili ya kuimarisha usalama. Ligi za nchi zilisimamishwa mapema mwaka huu kufuatia vurugu zilizotokea katika mji wa Port Said wakati wa mchezo baina ya timu ya Al Masr na Al Ahly na kusababisha watu zaidi ya 74 kupoteza maisha.

No comments:

Post a Comment