Wednesday, June 13, 2012

GABRIEL MILITO KUSTAAFU SOKA.

BEKI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Independiente ambaye anaandamwa na majeruhi ya mara kwa mara amemua kustaafu kucheza soka baada ya msimu wa Ligi Kuu nchini humo kumalizika. Beki mwenye umri wa miaka 31 ambaye pia amewahi kucheza katika klabu ya Barcelona ya nchini Hispania alikuwa na matarajio ya kupona wakati timu yake ya Independiente ilipokuwa ikikabiliwa na michezo miwili migumu lakini ilishindikana kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Gabriel ambaye ana undugu na mshambuliaji wa Inter Milan ya Italia Diego Milito alianza soka lake akiwa na klabu hiyo mwaka 1997 na kuisaidia kunyakuwa taji la Ligi Kuu ya nchini humo mwaka 2002 kabla kuhamia Hispania katika klabu ya Real Madrid. Akiwa Madrid alishindwa kufaulu vipimo vya afya na badala ya kuhamia klabu ya Real Zaragoza ambapo alicheza kwa misimu minne na kuisaidia timu hiyo kunyakuwa Kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid mwaka 2004. Baadae mwaka 2007 alihamia Barcelona na alikuwa katika kikosi ambacho kilinyakuwa taji la klabu bingwa ya Ulaya mwaka 2009 na 2011 na mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini Hispania lakini alishindwa kuendelea kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yaliyokuwa yakimsumbua na kuamua kurejea katika klabu yake ya nchini kwao ambayo ndio yuko nayo mpaka leo.

No comments:

Post a Comment