Thursday, June 14, 2012

LEO KATIKA HISTORIA: KAMANDA MUHAMMAD ALI TASHA ASHAMBULIA SUDAN


 1820
Miaka 192 iliyopita katika siku kama ya leo wanajeshi wa Misri wakiongozwa na kamanda Muhammad Ali Pasha waliishambulia Sudan na kulikalia kwa mabavu eneo kubwa la ardhi ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo Waingereza pia walilishambulia eneo la kusini mwa Sudan na kulikalia kwa mabavu. Hata hivyo wananchi wa Sudan wakiongozwa na Mahdi Sudani mwaka 1881 walianzisha harakati ya ukombozi dhidi ya uvamizi wa Misri na Uingereza na mwaka 1885 wakafanikiwa kutoa pigo kubwa kwa vikosi vamizi vya Misri na Uingereza na hivyo kulikomboa eneo kubwa la nchi hiyo yao.

No comments:

Post a Comment