Thursday, June 14, 2012

EPL NEWS: REDKNAPP ATIMULIWA KAZI SPURS


Siku ya leo ni Mbaya kuwahi kutokea kwa Kocha Harry Redknapp baada ya kutimuliwa kazi na Tottenhma Hostpur.

Harry mwenye miaka 65 jana alisisitiza kwamba ataendelea kuwepo White Hart Lane, lakini jioni hii alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy na hatimaye akatimuliwa.

Kocha huyo wa zamani wa West Ham alifanya mazungumzo na bosi wake Levy ili kuweza kujua hatma yake baada ya mkataba wake kuwa umebakiza miezi 12 uishe, huku akiwa na akiwa anajiamini amefanya kazi nzuri ambayo ingempa nafasi ya kuongezewa mkataba.

Lakini Levy inasemekana hakuwa na furaha na suala la Redknapp kushindwa kuiwezesha timu kupata nafasi ya champions league pamoja na kukaa kwenye nafasi ya tatu kwa muda mrefu kwenye msimamo wa ligi ya msimu uliopita.

Spurs walimaliza nafasi ya nne katika EPL,  kwa maana waliweza kupata nafasi nafasi lakini wakaikosa nafasi hiyo baada ya Chelsea waliokuwa nyuma yao kubeba ubingwa wa ulaya jijini Munich dhidi Bayern.

Mpaka sasa Redknapp bado anafanya mazungumzo ya juu ya mapato yake atakayoyapata baada ya Spurs kumtimua akiwa bado na mkataba wa mwaka 1, na anatagemewa kutangazwa rasmi kutimuliwa hapo kesho.

David Moyes wa Everton anatajwa kuwa ndio kocha anayeweza kumrithi Harry Redkanpp pale White Hart Lane.

No comments:

Post a Comment