Wednesday, June 20, 2012

KONA YA MWALIMU: KUBALI KUFUNDISHWA


K
ATIKA maisha kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wengine lakini kuna wengine hujiona kuwa wanajua kila kitu katika maisha yao, Kumbuka kwamba Mwanadamu ameumbwa na Nafsi, Roho na Mwili na kila kimoja kinahitaji usawa katika mahitaji yake.

Kwa kusema hivyo naamanisha kuwa Binadamu sio zalio la mazingira yake kwani kumekuwa na nadharia mbalimbali kwamba alitokea kwa nyani lakini iweje mwanadamu huyu huyu aanze kuabudu jiwe alilolifanya kwa mikono yake mwenyewe hapo ndipo utakapojua kwa kila kitu kinahitaji usawa.

Jifunze kutoka kwa wengine ili uweze kufaidika katika dunia hii na usione haya kuuliza kitu chcochote kwa mtu yoyote yule hiyo husaidia sana kufikia malengo.


No comments:

Post a Comment