Thursday, June 7, 2012

GLOBAL POLITICAL NEWS: SCO YAPINGA MASHINIKIZO DHIDI YA IRAN


Nchi 6 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) zimetoa taarifa ya pamoja na kusema kuwa zinapinga mashinikizo yoyote ya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uingiliaji wowote wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Taarifa hiyo ya pamoja imetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa SCO leo Alhamisi mjini Shanghai, China. Nchi hizo 6 ambazo ni China, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Tajikistan, na Uzbekistan zimesema mazungumzo ndiyo njia pekee ya kutatua kadhia ya nyuklia ya Iran pamoja na mgogoro wa kisiasa nchini Syria. Rais Hu Jin Tao wa China amesema kwenye hotuba ya ufunguzi kwamba nchi yake itatoa msaada wa dola bilioni 10 kwa nchi wanachama ili kusaidia miradi ya maendeleo na kuimarisha vita dhidi ya ugaidi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, India, Mongolia, Afghanistan na Pakistan zinahudhuria mkutano huo kama wanachama watazamaji.

No comments:

Post a Comment