Monday, June 11, 2012

GLOBAL NEWS: KUSIFIWA PINOCHET KWASABABISHA MAANDAMO CHILE

K
uonyeshwa kwa filamu mpya inayompongeza kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Chile Augusto Pinochet, kumesababisha maandamano ya mamia ya wakosoaji katika mji mkuu Santiago.
 
Polisi imesema  waandamanaji  64 wamekamatwa, na kutumia hewa ya kutoa machozi kufika katika jumba la sinema ambako mamia ya wafuasi wa Pinochet walikuwa wakiangalia filamu hiyo. Zaidi ya watu 3,200 waliuawa au kutoweka wakati wa  utawala wa  dikteta huyo baina ya  mwaka 1973 na 1990. Filamu hiyo inamuonyesha kuwa ni shujaa aliyeinusuru Chile dhidi ya Ukoministi. Pinochet alikufa  mwaka 2006, bila ya kuhukumiwa kwa  matukio ya ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binaadamu wakati wa utawala wake.

No comments:

Post a Comment