Monday, June 25, 2012

GATLIN, GAY WAFUZU OLIMPIKI MBIO FUPI.

Justin Gatlin.
WANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Marekani Justin Gatlin na Tyson Gay wamefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London baada ya kutumia wa sekunde 9.90 katika majaribio ya kikosi cha nchi hiyo. Gatlin ambaye amewahi kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka 2004 alifanikiwa kutumia muda wa sekunde 9.80 mbele ya Gay ambaye alitumia sekunde 9.86 katika mbio hizo za majaribio. Katika kikosi hicho cha Marekani mwanariadha Ryan Bailey alimaliza mbio hizo katika nafasi ya tatu akitumia muda wa sekunde 9.93 akifuatiwa na Michael Rodgers huku tano bora ya timu hiyo ikihitimishwa na Darvis Patton aliyetumia muda wa sekunde 9.96. Michuano hiyo ya olimpiki itakuwa ni ya kwanza kwa Gatlin kushiriki toka ile iliyofanyika Athens ambapo alikosa michuano ya 2008 iliyofanyika Beijing kutokana na kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu. Hatma ya ushiriki wa michuano ya olimpiki kwa mwanariadha nyota wa mbio hizo kutoka Uingereza Dwain Chambers imekuwa haijulikani baada ya mwanariadha huyo kuondolewa katika mbio hizo za majaribio zilizofanyika jijini Helsinki, Finland. Chambers alishindwa kuwika katika mbio za majaribio za zilizofanyika Birmigham mwezi uliopita baada ya kutumia muda wa sekunde 10.04 na ili afuzu michuano ya olimpiki lazima atumie muda wa chini ya sekunde 10 katika mashindano yoyote kabla ya Julai 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment