Sunday, June 24, 2012

EURO 2012 NEWS: YOHANA NA ISMAIL WAIBUKA KIDEDEA EURO VIBE FANS ZONE


W
ashindi wa zawadi ya EURO VIBE FANS ZONE wamejinyakulia zawadi zao kwa mara nyingine tena katika usiku wa Juni 24 mwaka huu baada ya kushinda Chemsha Bongo ya kujibu maswali kuhusu mechi kati ya England na Italia iliyochezwa usiku wa kuamkia leo. 

Chemsha bongo hiyo iliyoendeshwa na Redio Mbeya FM iliwaleta pamoja wadau wa soka katika michuano ya EURO 2012 Jijini Mbeya inayoendelea nchini Poland-Ukraine imefanyika katika Ukumbi wa nje wa Vibe Club (Vibe Outdoor).

Yohana na Ismail wote wakazi wa Jiji la Mbeya wamejnyakulia jezi za timu ya England na kuhojiwa moja kwa moja na kituo cha Redio Mbeya kuhusu mechi hiyo iliyomalizika kwa Italia kufuzu katika hatua ya Nusu baada ya kumchapa England kwa penati  4-2 .

Italia atakutana na Ujerumani katika Nusu Fainali siku ya Alhamisi.


No comments:

Post a Comment