Sunday, June 17, 2012

CAMEROON, NIGERIA ZASONGA MBELE, TANZANIA!!??

MABINGWA wa zamani wa Afrika timu za Cameroon na Nigeria jana zimefanikiwa kusonga mbele katika michezo yao ya kufuzu michuano hiyo ambayo itafanyika Afrika Kusini mwaka kesho lakini zote zikipata ushindi mwembamba. Cameroon walifanikiwa kuifunga Guinea Bissau bao 1-0 katika mchezo uliochezwa jijini Younde na kufanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda bao 1-0 pia. Nigeria ambayo ilikipiga na Rwanda jijini Calabar ilifanikiwa kuifunga timu hiyo kwa mabao 2-0 na kufanikiwa kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza ulipigwa jijini Kigali timu kutoka suluhu ya bila ya kufungana. Nchi hizo zimeungana na Cape Verde Islands, Malawi, Liberia, Sierrs Leone na Uganda katika hatua inayofuata ya kufuzu mchuano hiyo. Kuna michezo mingine saba ya mzunguko wa kwanza ambayo inatarajiwa kupigwa leo ambapo timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars itakuwa wageni wa Msumbiji katika mchezo utakaochezwa leo jioni jijini Maputo.

No comments:

Post a Comment