Friday, June 22, 2012

BOCA JUNIORS KUCHEZA FAINALI NA CORINTHIANS, COPA AMERICA.


 

KLABU ya Boca Juniors ya nchini Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Universidad ya Chile katika mchezo uliochezwa jana. Boca ambao ni mabingwa wa michuano hiyo mara sita walitinga hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya mchezo wa kwanza kufanikiwa kuifunga Universidad katika Uwanja wa La Bombonera jijini Buenos Aires, Argentina. Sasa Boca wanatarajiwa kukutana na Corinthians ya Brazil ambao walifanikiwa kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo Santos kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa jumatano. Katika fainali ya michuano hiyo itakayochezwa nyumbani na ugenini Boca Juniors itakuwa ikicheza fainali yake ya 10 katika michuano hiyo huku Corinthians wenyewe ikiwa ni fainali yao ya kwanza toka waanze kushiriki michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment