Thursday, June 28, 2012

BECKHAM ATEMWA KIKOSI CHA OLIMPIKI.

KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza ametemwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London mwaka huu. Beckham mwenye ana umri wa miaka 37 amewahi kuwa nahodha wa nchi kipindicha nyuma na alikuwa akitaka nafasi katika kikosi hicho kitakahoshiriki olimpiki kabla ya kuamua kutundika daluga. Akihojiwa mara baada ya kutangazwa kwa kikosi hicho Beckham amesema kuwa amesononeshwa na kuachwa kwake kwenye kikosi hicho lakini bado ataendelea kuwa mshabiki wa timu hiyo katika michuano hiyo na anaamini wataibuka kidedea na kunyakuwa medali ya dhahabu. Kocha wa kikosi hicho Stuart Pearce alimuingiza mchezaji huyo katika orodha ya wachezaji 35 lakini katika mchujo ili kubakia na kikosi cha mwisho cha wachezaji 18 kocha huyo alimchagua beki Micah Richards badala yake. Pearce alimpigia simu Beckham kumtaarifu hatomjuisha katika kikosi hicho kwakuwa alikuwa akihitaji kutengeneza kikosi ambacho kitakuwa cha kujihami zaidi katika michuano hiyo ndiyo maana akaamua kumchukua beki Manchester City Richards ili kusaidia kwenye suala la ulinzi.

No comments:

Post a Comment