Thursday, June 28, 2012

BARCELONA YAPATA MBADALA WA ABIDAL.

KLABU ya Barcelona imejipanga kujizatiti kwenye safu ya ulinzi msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata mbadala wa aliyekuwa beki wa klabu hiyo Eric Abidal ambaye ni mgonjwa kwa kumsajili beki wa klabu ya Valencia Jordi Alba kwa mkataba wa miaka mitano. Katika taarifa za klabu hiyo ambazo zimetumwa katika mtandao wa kijamii wa twitter Alba mwenye miaka 23 ambaye kabla ya kwenda Valencia alikulia katika shule ya watoto ya Barcelona amesajiliwa kwa ada ya euro milioni 14 baada ya kufaulu vipimo vya afya. Barcelona imekuwa sokoni kwa kipindi kirefu ikijaribu kutafuta beki ambaye ataziba pengo la Abidal ambaye amefanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini mapema mwaka huu na haijulikani kama beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa atarejea tena uwanjani baada ya kupona. Alba ambaye pia yuko katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania alianza kuichezea nchi hiyo Octoba mwaka jana ambapo aliitwa kuziba pengo la Joan Capdevila katika mchezo dhidi ya Scotland na toka kipindi hicho hajaachwa kwenye kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment