Tuesday, June 12, 2012

AFRICA NEWS: KENYA NA IRAN ZATILIANA SAINI


Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya zimetiliana saini makubaliano ya kurejesheana wahalifu wa pande mbili.
Taarifa iliyotolewa na kituo cha upashaji habari cha Rais wa Iran imeeleza kwamba Wizara ya Sheria ya Iran inapaswa kushughulikia makubaliano hayo yaliyotiwa saini kati yake na Kenya kuhusiana na kurejesheana wahalifu wa pande mbili na kufuatilia mwenendo wake wa kisheria hadi utakapopasishwa. Kwa kutiwa saini makubaliano hayo, nchi hizo mbili pia zimeafikiana kupanua ushirikiano na uhusiano wao kwa msingi wa kujitawala mataifa, kutoingilia masuala ya ndani ya upande wa pili na kulinda maslahi ya nchi hizo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Iran na Kenya zitawajibika kuwakamata katika nchi zao raia wa upande wa pili watakaofanya jinai au wanaotafutwa na vyombo vya sheria vya nchi hizo mbili na kuwakabidhi.

No comments:

Post a Comment