Saturday, June 23, 2012

YANGA YAMUACHA ASAMOAH.HATIMAYE klabu ya soka ya Yanga imeamua kuamuachia mshambuliaji wake Keneth Asamoah baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili. Asamoah alifikia makubaliano na Yanga kuhusu kuondoka kwake ambapo klabu hiyo inatarajiwa kumlipa fidia kutokana na kusitisha mkataba wake ambao alisaini msimu uliopita. Asamoah ambaye ana miaka 24 alijiunga na Yanga akitokea klabu ya FK Jagodina ya Serbia mwaka 2010 na alifungwa bao la kukumbukwa dhidi ya Simba katika michuano ya Kombe la Kagame mwaka 2011. Mchezaji huyo pia ameshinda taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2010-2011 akiwa na klabu hiyo na msimu uliopita alimaliza akiwa amefunga mabao 10.

No comments:

Post a Comment