Monday, June 25, 2012

WAZIRI POLAND ASIKITISHWA UINGEREZA KUTOLEWA.

Joanna Mucha.
WAZIRI wa michezo nchini Poland, Joanna Mucha ameonyesha masikitiko yake makubwa baada ya timu ya taifa ya Uingereza kuenguliwa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Italia. Mucha amesema kuwa amesikitishwa kwakuwa mashabiki wengi watarejea nchini kwao kutokana na kutolewa kwa nchi hiyo kwenye michuano hiyo. Waziri huyo kijana mwenye umbo la kuvutia aliendelea kusema kuwa kama Uingereza wangeshinda wangevutia mashabiki wengi zaidi kujitokeza katika nusu fainali dhidi ya Ujerumani ambao ungefanyika jijini Warsaw, Poland. Mucha amesema kuwa wakati wa mchezo baina ya Uingereza na Italia alikuwa akiomba Uingereza washinde ili waweze kusonga mbele lakini haikuwa hivyo katika dua zake.

No comments:

Post a Comment